Like Us

Z Anto amjibu Stamina kwa wimbo “Diamond na Alikiba waliachwa wakauchuna”

Msanii wa muziki, Z Anto amejibu mapigo baada ya kuusikiliza wimbo wa Stamina ‘Asiwaze’ ambao ulizua gumzo baada ya rapa huyo kudai alichokiimba kina uhalisia katika maisha yake. Z ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo Mpenzi Jini, amemtaka rapa huyo kuacha kulalamika huku akitolea mfano Diamond kuachwa na Zari, pamoja na Alikiba kuachana na mama watoto wake, Amina ambaye ni raia wa Kenya. 
Stamina wakati anahojiwa na vyombo mbalimbali vya habari alikiri kwamba wimbo huo, matukio mengi yanaukweli kuhusu maisha yake huku akiwataka vijana wenzake wasiache kuona kutokana na historia aliyoipitia.

Chanzo Bongo5 

Post a Comment

0 Comments