Like Us

Moto wa Harmonize hauzimiki aachia Nyimbo TATU ndani ya siku MBILI, Moja akimshirikisha msanii wa Nigeria

Msanii wa Bongo Fleva na C.E.O wa Konde Gang Harmonize ameuwasha moto kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kuachia video mbili za nyimbo zake pamoja na audio mpya ya Hujanikomoa.
Harmonize aliachia video ya wimbo wa ‘HAUNISHTUI’ licha ya audio yake kuachiwa wiki kadhaa nyuma lakini Video imeachiwa siku ya jana ya januari 4/2020.
Mapema Tarehe 05/01/2020 Harmonize ameachia video ya wimbo wake mpya “TEPETE” akimshirikisha msanii kutoka nchini Nigeria Mr Eazi.
Usiku huo wa tarehe 05/01/2020 Harmonize aliachia nyimbo nyingine yenye utofauti zaidi na alivyozoeleka SINGELI iitwayo Hujanikomoa

Post a Comment

0 Comments