Like Us

SAMATTA kwa mara ya KWANZA Aipatia Aston Villa BAO la KICHWA Premier League Msimu huu

Kwa mara ya kwanza msimu huu klabu ya Aston Villa imefanikiwa kufunga bao la kichwa kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Tanzania, Mbwana Samatta.

Bao hilo la kichwa ndiyo la kwanza kwa klabu ya Aston Villa kunako Premier League msimu huu kwa mujibu wa Mtangazaji wa shirika la habari la Sky Sports.
Mchezo wa Villa hapo jana dhidi ya Bournemouth ni wa 25 kunako Premier League lakini inaelezwa angalau nyota huyo Samatta amefunga bao la kichwa.
Licha ya kupata bao hilo lakini Villa ilijikuta ikimaliza dakika 90 bila ya kuondoka hata na pointi mmoja baada ya kuadhibiwa kwa jumla ya mabao 2 - 1 na Bournemouth.

Hata hivyo nyota huyo alifanikiwa kutimiza moja ya wajibu wake kama Mshambuliaji kwa kufunga huku mwenyewe alipohojiwa baada ya mechi amesema kuwa amejisikia vibaya kupoteza pointi tatu kwa kuwa ndiyo hitaji ya timu.

Aston Villa ipo nafasi ya nne kutoka chini katika timu zinazotakiwa kushuka daraja, ikiwa na jumla ya pointi 25 nafasi ya 17, wakati West Ham wakiwa wa 18 na alama 24, Watford wa 19 na pointi zao 23 huku Norwich City ikiburuza mkia kwenye msimamo wa Premier League wakiwa na alama 18.

Post a Comment

0 Comments